Mama kichwa cha familia Simiyu

SIMIYU: Mkoa wa Simiyu kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), kupitia matokeo ya Sensa na watu na makazi 2022, unaongoza kwa kaya nyingi zinazoongozwa na wanawake kulinganisha na mikoa mingine Tanzania nzima.

Kwa mujibu wa Matokeo hayo ya sensa 2022, Mkoa huo unazo jumla ya Kaya 317,963 ambapo asilimia 42.5 ya kaya hizo zinazoongozwa na wanawake.

Mtakwimu kutoka Ofisi ya Taifa Takwimu (NBS) Pastory Ulimali, akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa mafunzo ya matokeo ya sensa kwa viongozi wa mkoa huo Mkoa huo ulionekana kuwa na kaya nyingi zinazoongozwa na wanawake kuliko mikoa mingine Tanzania nzima.

“ Kwa takwimu za Kaya kwa mkoa wa Simiyu ambapo ni Kaya 317,963, asilimia 57.5 ya kaya hizo zinaongozwa na wanaume na asilimia 42.5 zinazoongozwa na wanawake,” alisema  Ulimali na kuongoza

“ Kwa takwimu hizo siyo kwamba mkoa wa Simiyu kaya nyingi zinazongozwa na wanawake, bali ukilinganisha na mikoa mingine Tanzania nzima, mkoa wa Simiyu unaongoza,”alisisitiza Ulimali.

Mtakwimu huyo alisema kuwa ni wakati sasa wa wataalumu wengine wa utafiti nchini, kufanya utafiti wa kina kujua ni kwa nini mkoa wa Simiyu unazo kaya nyingi ambazo zinaongozwa na wanawake.

“ Wakati wa zoezi la Sensa, sisi tulikuwa tunauliza swali moja tu, Nani Mkuu wa Kaya hapa, hatukuuliza sababu za hizo kaya kuuongozwa na wanawake, ni wakati wa walaamu wengine sasa kufanya utafiti kujua sababu,” alisema Ulimali.

Mejena Takwimu Mkoani humo Suzana Kulindwa alisema kuwa hivi sasa serikali inatekeleza awamu ya tatu ya mwisho ya matokeo ya sensa ya watu na makazi 2022.

Alisema katika awamu hii kazi zinazofanyika ni pamoja na uchakataji, uchambuzi, uandishi wa ripoti mbalimbali za sensa, na usambazaji na mafunzo ya matumizi ya matokeo ya sensa.

“ Serikali imekamilisha kuandaa na kuzindua ripoti 11 za sensa ikiwa pamoja na ile ya matokeo ya mwanzo, ripoti hizo zimejikita katika mgawanyo wa idadi ya watu, kwa maeneo ya kiutawala hadi ngazi ya kata, Halmashauri, majimbo Tanzania bara na Zanzibar” alisema Kulindwa.

Habari Zifananazo

Back to top button