Mama mbaroni akidaiwa kuua mwanawe wa miaka 4

JESHI la Polisi mkoani Mtwara linamshikilia mwanamke Mwazanije Dadi, mwenye umri wa miaka 34, akidaiwa kumuua mtoto wake Najma Ahmad mwenye umri wa miaka 4.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Nicodemus Katembo, amesema mwanamke huyu alitenda kosa hilo Desemba 12, 2022 Kijiji cha Sinde, Kata ya Msanga Mkuu wilayani Mtwara.

Katembo amesema mwanamke huyu alimkaba mtoto huyu shingoni hadi kusababisha kifo chake.

“Baada ya uchunguzi wa kitabibu uliofanywa na daktari, ilibainika kuwa chanzo cha kifo cha mtoto ni kukosa hewa ‘suffocation’ baada ya kukabwa,” amesema.

Amesema mwanamke huyo kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi na atafikishwa mahakamani, mara baada ya uchunguzi kukamilika kwa hatua za kisheria zaidi.

Habari Zifananazo

Back to top button