Mama na mtoto wakumbukwa bima za afya

MWANZA: KATIKA kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za Serikali kwenye utoaji  wa huduma bora za afya Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tazania imetoa jumla ya bima kubwa 200 za matibabu kwa wakinamama na watoto katika wodi ya wazazi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa kampeni ya sambaza shangwe gusa maisha iliyofanyika katika stendi ya Posta jijini Mwanza Meneja mauzo mwandamizi wa Vodacom Kanda ya ziwa ,Straton Mchau amesema kuwa kupitia kampeni ya sambaza shangwe gusa maisha wametembelea Hospitali ya Sekou Toure na kutoa bima kubwa za matibabu kwa wakinamama waliojifungua pamoja na watoto.

“Pamoja na hayo  tumeona ni kitu cha muhimu sana haswa katika msimu huu wa sikukuu kuwasaidia vijana au watoto waweze kukua katika maisha mazuri na kuwa na afya njema ndio maana bima imekuwa ni kitu cha msingi kuwapatia wakinama pamoja na watoto wao” Alisema

Godfrida Frederick ni mkazi wa Nyegezi Jijini Mwanza ambaye ameshida zawadi ya Tv katika kampeni hiyo ameishukuru kampuni ya Vodacom kwa kuja na kampeni ya sambaza shangwe gusa maisha pamoja na kujitoa kwako katika kusaidia jamii kupitia kampeni tofauti tofauti .

Kwa upande wake, Simon Bundala Mkazi wa Nyang’wale Mkoani Geita aliyeibukuka mshindi wa Sh milioni 10 katika kampeni ya sambaza shangwe gusa maisha ameishukuru kampuni ya Vodacom na kusema kuwa pesa alizopata zitamsaidia kuendeleza shughuli zake za kilimo pamoja na kusomesha watoto.

 

Habari Zifananazo

Back to top button