Mama wa Luiz Diaz apatikana
TAARIFA zinaeleza mama mzazi wa mchezaji wa Liverpool, Luis Diaz anayejulikana kwa jina la Cilenis Marulanda amepatikana akiwa hai baada ya taarifa za kutekwa jana.
–
Ripoti kutoka vyanzo mbalimbali jana vililipoti kuwa baba na mama wa mchezaji huyo walitekwa huko Colombia.
–
Taarifa ya mwandishi wa habari, Fabrizio Romano imeeleza kuwa polisi wanaendelea kumtafuta baba wa mchezaji huyo.
#LIVERPOOL #Diaz