LINDI; WAKALA wa Barabara (TANROADS) kwa kushirikiana na wataalamu wa Wizara ya Ujenzi na wakandarasi wamefanikiwa kurejesha mawasiliano ya barabara kwenye eneo la Somanga lililoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha kwenye baadhi ya maeneo nchini.
Hadi kufikia asubuhi ya leo Mei 8, 2024 kazi ya urejeshaji wa miundombinu ya barabara hiyo katika eneo la Somanga imefikia hatua za ukamilishaji, hivyo kuruhusu magari yanayobeba mawe kupita eneo hilo na kuelekea kwenye maeneo mingine yaliyoathiriwa na mvua kwa ajili ya ukarabati.
Isome pia:https://habarileo.co.tz/mawasiliano-barabara-lindi-dar-yarejea/
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya Ujenzi, nguvu ya timu ya wataalamu wa TAiNROADS kwa kushirikiana na wakandarasi inaelekezwa kwenye urejeshaji wa miundombinu ya barabara katika eneo la Songas lililopo barabara kuu ya Lindi – Dar es Salaam, ambalo pia lilikatika kutokana na mvua kubwa zilizonyesha na kuambatana na kimbunga Hidaya.