PROMOTA maarufu wa masumbwi Bob Arum anavutiwa na mpango wa kuandaa pambano kati ya bingwa wa mikanda ya IBF, WBC na WBO Artur Beterbiev na moja kati ya mabondia wawili Canelo Alvarez au David Benavidez.
Promota huyo anasema ameshawishika na wazo la bondia Beterbiev la kutaka kuzichapa na mabondia hao, hivyo anaamini ni wakati sahihi wa kuandaa pambano hilo.
Bondia Artur Beterbiev atalazimika kujipanga kwanza na pambano lake la mwezi Agost mwaka huu dhidi ya Callum Smith, japo promota Arum amesisitiza kuwa hata akipoteza pambano dhidi ya Smith bado kiu ya bondia huyo ni kupambana na Alvarez au Benavidez.
Bado hakuna uhakika juu ya pambano hilo kufanyika, kwani imeripotiwa kuwa Canilo Alvarez amepewa ofa nono ili akubali kupambana na David Benavidez, ambapo kama pambano hilo litafanya uwezekano wa Beterbiev kupata pambano kuwa mgumu.