Mambo safi mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Uganda

TANGA: Kamati ya Kudumu ya bunge ya Nishati na madini imeridhishwa na utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka nchini Uganda katika eneo la Chongoleani Jijini Tanga.

Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya ziara ya kamati hiyo kutembelea eneo la mradi ambalo litajengwa matanki ya kuhifadhi mafuta ghafi na gati Mwenyekiti wa kamati hiyo David Mathayo alisema kuwa mradi huo utakapokamilika utakuwa na manufaa makubwa ya kiuchumi Kwa nchi.

Amesema kuwa mradi huo ni miongoni mwa miradi mikubwa duniani hivyo wameridhishwa na kasi ya utekelezaji wake na namna ambavyo serikali imekuwa ikishiriki kwa ukamilifu kwenye mradi huo.

Advertisement

“Ni mradi ambao utakapomalizika watanzania utaweza kutunufaisha sana hivyo rai yetu sisi wabunge mradi huu uendelee kwani ni mzuri sana”amesema Mwenyekiti huyo.

Hata hivyo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya nishati Athumani Seleman amesema kuwa zaidi ya watanzania 4228 sawa na asilimia 91 wameweza kunufaika na fursa za ajira katika mradi huo.

Amesema kuwa  zaidi ya watoa huduma 146 wamenufaika kwa kupata malipo kutokana na kutoa huduma mbalimbali kwa kiasi cha Sh bilioni 355.

“Tayari Dola milioni 207 zimelipwa kwa ajili ya hisa kwenye mradi huo kati ya Dola milioni 308 ambazo zilitakiwa kulipwa kwa ajili ya hisa za mradi huo”amesema Naibu Katibu Mkuu huyo.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *