Mambo safi MV Mwanza

MWANZA: Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Meja Jenerali Paul Simuli, ametembelea mradi wa ujenzi wa meli ya MV Mwanza Hapa Kazi Tu inayotarajiwa kuanza kazi katikati ya mwaka huu.

Balozi huyo amesema meli hiyo itasaidia kuongeza shehena ya Tanzania kwenda Uganda, kutoka asilimia mbili za sasa, pia inatarajiwa ongezeko la shehena hasa ya mchele, ambayo ni mojawapo ya bidhaa pendwa nchini Uganda..

“Tunatambua sio meli ya kubeba shehena peke yake, lakini hicho kiasi cha mizigo itakachokuwa ikibeba kitaongeza wasafirishaji kwasababu Waganda wanachohitaji ni usafiri wa uhakika tu,”amesema.

“Kwakweli serikali imefanya kitu kikubwa cha kuipa heshima Tanzania na hata mimi binafsi huko Uganda. Tumepanga kuwaalika Waganda wengi iwezekanavyo kushuhudia meli hii siku itakapotia nanga katika Bandari ya Port Bell.

Habari Zifananazo

Back to top button