Mambo ya Nje waomba bajeti Sh Bil 241

DODOMA; WIZARA ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imeomba kuidhinishiwa jumla ya Sh 241,069,232,000 kwa Mwaka wa Fedha 2024/25.

Akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2024/25 mjini Dodoma leo, Waziri January Makamba, amesema kati ya fedha hizo Sh 229,435,856,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh 11,633,376,000 ni kwa ajili ya bajeti ya maendeleo.

“Vilevile, Wizara imepanga pia kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo yenye makisio ya thamani ya Sh 343,100,000,000 kutoka vyanzo mbadala ikiwemo ubia na mikopo ya karadha.

“Fedha hizo zinajumuisha Sh 127,000,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi na kitega uchumi Nairobi, Kenya; Sh 66,100,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi, makazi ya Balozi na vitega uchumi Lusaka, Zambia na Sh 150,000,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi, makazi ya balozi na kitega uchumi Kinshasa, DRC,” amesema Waziri Makamba.

Habari Zifananazo

Back to top button