Mambo yaanza Miss Pwani 2023

Mkoa wa Pwani umezindua rasmi kuanza kwa shindano la Miss Pwani mwaka 2023.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Pwani, Mratibu wa shindano hilo, Irene Shirima amesema fomu za wanaowania zinaanza kutolewa leo Februari 17, 2023.

“Dirisha la kuchukua fomu limezinduliwa rasmi leo na litafungwa  Aprili 12, 2023  huku usaili unatarajiwa kufanyika Aprili 15, mwaka huu.

“Mshiriki anatakiwa kuwa  na umri wa miaka 18 hadi 24, asiwe ameolewa wala kuwa na mtoto,” amesema.

Kwa upande wake Ofisa Utamaduni Mkoa Pwani,  Nanyuni Sironga, amewaomba wakazi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi hio.

Amesema mkoa huo utaendelea kufuatilia na kuunga mkono mshindano hayo, ili yafanyike kwa ufanisi mkubwa.

Habari Zifananazo

Back to top button