Mambo yaiva TASWA Media Day Bonanza

DAR ES SALAAM; CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA),kimetangaza kuwa bonanza la waandishi litakalofanyika Desemba 16, 2023 litakuwa na michezo mbalimbali, hivyo kuwataka waandishi kujipanga kushiriki michezo hiyo.

Taarifa ya Katibu Mkuu wa TASWA iliyotolewa leo Alhamisi Oktoba 26, 2023 imeeleza kuwa tamasha hilo linalojulikana kama ‘TASWA Media Day Bonanza 2023’ litafanyika Msasani Beach Klabu jijini Dar es Saalam na kutaka kila atakayehudhuria ahakikishe angalau anashiriki mchezo japo mmoja.

“Michezo inayotarajia kuwepo ni riadha, ambayo itahusisha mbio za mita 100, mbio za kupokezana vijiti, kutembea haraka, kuruka chini, kukimbia na gunia, kukimbia na yai kwenye kijiko na kukimbia na glasi yenye maji.

“Michezo mingine ni mpira wa miguu, mpira wa kikapu, mpira wa wavu, mpira wa pete, kurusha tufe, kuvuta kamba, kuruka kamba, mchezo wa vishale, mpira wa meza, draft, mchezo wa pool  table, mchezo wa bao, karata, rede, mdako, kupenya ndani ya pipa, kushindana kucheza muziki, kushindana kunywa soda, kushindana kufukuza kuku na kushindana kula ugali na kuku mzima wa kuchoma,” amesema Lucas.

Amesema michezo hiyo sehemu kubwa  ni ya kujifurahisha si ya ushindani, hivyo haihitaji kutafuta watu ambao si wafanyakazi wa vyombo vya habari waje kusaidia na kueleza kuwa wanatarajia waandishi wa habari za aina zote pamoja na wafanyakazi wa vyombo vya habari zaidi ya 2000 watahudhuria.

 

Habari Zifananazo

Back to top button