Mambo yaiva ujenzi Vituo Jumuishi vya mahakama

DAR ES SALAAM; SERIKALI imesaini mikataba na kampuni nne yenye thamani ya  Sh bilioni 49  kwa lengo la  kujenga  vituo sita  jumuishi vya kutoa huduma za mahakama.

Akizungumza leo Novemba 3, 2023 jijini Dar es Salaam, wakati wa kusaini mikataba hiyo, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel,  ametaka mikoa ambayo vitajengwa ni Njombe, Katavi, Geita, Simiyu, Songea na Songwe.

Prof. Gabriel amesema ana imani kuwa wakandarasi waliopewa jukumu hilo watafanya kazi kwa weledi na kwa muda waliowekewa wa miezi tisa na kwamba mahakama haitosita kumchukulia hatua mkandarasi yeyote atakayekuwa kikwazo kufanikisha malengo hayo

Kwa upande wake mwakilishi wa waliosaini mkataba huo Mhandisi Kapinga S.Kapinga Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Azhar Construction, ameahidi kufanya kazi kwa weledi na kwamba hawatawaangusha katika ujenzi huo.

Ujenzi huo wa vituo jumuishi vya kutoa huduma ya mahakama ni wa awamu, hivyo bado serikali inaendelea na mchakato wa kujenga vituo vingine malengo ni vituo 14.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button