Mambo yameiva tamasha la dansi Mbeya

WASANII wa muziki wa dansi nchini wameahidi kukonga nyoyo za mashabiki katika onesho lao Agosti 7, 2023 kwenye mkesha wa maadhimisho ya sikukuu ya wakulima ‘Nanenane’ jijini Mbeya.

Muandaaji wa tamasha hilo Mboni Masimba amesema kwa muda mrefu hakuwahi kufanya tamasha mkoani humo, hivyo siku hiyo patachimba ukumbi wa Tughembe.

Amewataja baadhi ya watakaotumbuiza kuwa ni bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ chini ya Ally Choki, bendi ya Msondo Ngoma pamoja na msanii Christan Bella.

Kwa upande wake Choki amesema wamejiandaa vizuri na kwamba mashabiki wajitokeze kupata burudani ya nguvu.

Naye Bella ametamba kuwa atawaburudisha mashabiki wake kwa nyimbo mpya pamoja na zile za zamani.

Habari Zifananazo

Back to top button