Rais wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan leo anatarajiwa kuzindua tukio la kujaza maji katika Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) baada ya ujenzi wake kufikia asilimia 78.68.-
Tukio hilo litakofanyika eneo la mradi, Dk Samia atabonyeza kitufe ambacho kitafunga handaki la kuchepusha maji, hivyo kuruhusu maji kuanza kuingia kwenye bwawa hilo la ujazo wa lita bilioni 32.-
Uzinduzi wa ujazaji maji ni utekelezaji wa mradi huo ambao utazalisha megawati 2,115 zitakazotosheleza mahitaji ya sasa na kuwa kichocheo cha uwekezaji nchini.-
Taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Maharage Chande, imesema kuwa uingizwaji wa maji unatarajiwa kukamilika mwaka 2024, na uzalishaji wa umeme utaanza Juni mwaka huo.