Mambo yamenoga miaka 36 ya TAMWA

RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 36 ya Chama cha Wanahabari Wanawake  Tanzania (TAMWA).

Maadhimisho hayo yamepangwa kufanyika Novemba 28 na 29 Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo Novemba 26, Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Dk Rose Reuben amesema pamoja na mambo mengine katika maadhimisho hayo pia watazindua jarida maalum la Sauti ya Siti ambalo lilisimama uchapishwaji wake tangu mwaka 2017.

“Pia tutazindua ripoti maalum ya rushwa ya ngono na ukatili wa kijinsia ndani ya vyombo vya habari,”amesema Dk Rose.

Amesema pia wanatarajia kutoa tuzo kwa mwanahabari aliyefanya viuzri katika masuala ya afya ya uzazi na kutoa zawadi maalum ya kutambua na kuthamini mchango wa waasisi 13 wa TAMWA.

Aidha Dk Rose amesema maadhimisho hayo yataakisi safari ya miaka 36 ya TAMWA ambayo imeendelea kujikita katika kuhamasisha upatikanaji wa haki za wanawake na watoto wa kike nchini.

“Maono ya TAMWA ni kuwa na jamii ya Kitanzania iliyo na amani na inayo Heshimu haki za binadamu kwa mtazamo wa kijinsia,”amesema.

 

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button