Mambo yamenoga michuano ya vijana Afrika
UNGUJA, Zanzibar: TIMU ya wavulana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 15 (U15) imepangwa Kundi A ya Michuano ya ‘African Schools Football Championship 2024’ zinazotarajiwa kutimua vumbi kuanzia Mei 21 hadi 24, mwaka huu katika Uwanja wa New Amaan Complex, kisiwani Unguja, Zanzibar.
Soma pia: https://www.instagram.com/p/C7LtvnruhBB/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==
Takribani Nchi 44 zimethibitisha ushiriki katika michuano hii, ambapo zaidi ya vijana 800,000 wake kwa waume U15 wanataraji kushindana kuwakilisha mataifa yao.
Vijana pia watapata fursa ya kupata mafunzo kutoka kwa wasakata kabumbu hodari barani Afrika, miongoni mwao ni Emmanuel Adebayor kutoka Togo, Daniel Amokachi kutoka Nigeria na mhambuzi nguli wa soka kutoka Afrika Kusini, mwanadada Amanda Dlamini.
Droo ya michuano hii imefanyika jana. Tazama makundi hapo juu.