Mambo yanoga Bandari za Ziwa Tanganyika

SHILINGI bilioni 108 zilizowekezwa na serikali katika uboreshaji wa bandari za ziwa Tanganyika, zimekuwa kichocheo kikubwa cha uchumi na biashara nchini kutumia fursa inayopatikana kwenye nchi za ukanda wa maziwa makuu.

Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Edward Mabula amesema hayo wakati wa kuhitimisha wiki ya maadhimisho ya miaka 18 tangu kuanzishwa kwa mamlaka ya usimamizi wa bandari na bandari za maziwa kusimamiwa na mamlaka hiyo.

Mkuu wa wilaya Kigoma Salum akizungumza wakati akihitimisha maadhimisho ya miaka 18 ya TPA. (Picha na Fadhil Abdallah).

Mabula amesema kuwa ziwa Tanganyika lina jumla ya bandari rasmi 18 zinazosimamiwa na TPA, ambapo kati yake bandari 10 zipo mkoa Kigoma, zimekuwa zikisafirisha mizigo na abiria kwenda ndani na nje ya nchi.

Advertisement

Amesema kuwa maboresho makubwa yaliyofanywa kwenye miundombinu ya bandari na vitendea kazi imezifanya bandari hizo kusafirisha mzigo mkubwa kwenda nje ya nchi kwenda nchi za Maziwa makuu, ambapo jumla ya tani 277,868 kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni mwaka huu na mpango ni kuongeza wigo wa kuhudumia shehena kufikia tani 300,000.

Akihitimisha maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya Kigoma, Salum Kali amesema kuwa serikali imefanya kazi kubwa kuhakikisha bandari hizo zinatoa tija inayowezesha kuongeza mapato ya nchi ikiwemo kuleta kiasi cha shilingi bilioni 32 kwa ajili ya uboreshaji huo.

3 comments

Comments are closed.