Mambo yanoga kuelekea Kombe la Dunia

IKIWA zimesalia wiki tatu kuelekea mashindano ya Kombe la Dunia nchini Qatar, Kampuni ya bidhaa za kielektroniki ya Life is Good ‘LG’, imezindua kampeni maalum ya kutoa punguzo la bei kwa wananchi watakaonunua bidhaa zake katika msimu huu wa Kombe la Dunia.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Jake Choo amesema kwa kipindi kirefu kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele kuwafikia Watanzania wengi kupitia bidhaa zake, na katika msimu huu wameamua kutoa punguzo hilo, ili Mtanzania wa kila hali aweze kufurahia ubora wa bidhaa zao.

Mkurugenzi wa Masoko wa chapa ya MO, Fatema Dewji amesema ushirikiano wao na kampuni mbalimbali za kimataifa ikiwemo LG, unalenga kuwapa Watanzania fursa ya kufurahia ubora wa viwango vya kimataifa.

Habari Zifananazo

Back to top button