Mambo yanoga mashindano gofu Lugalo

MASHINDANO YA gofu la kumuenzi Mkuu wa Majeshi ‘NMB CDF TROPHY 2023’ yanatarajiwa kufanyika  Septemba 2 na 3 mwaka huu katika Klabu ya Gofu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lugalo jijini Dar es Salaam.

Akizunguza Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa klabu ya gofu Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo amesema mbali na Shindano hilo la kumuenzi Mkuu wa Majeshi vilevile litatumika kuenzi siku ya kuzaliwa kwa JWTZ.

“Tutasherekea kuzaliwa kwa  JWTZ, sherehe zitaambatana na shindano la NMB CDF TROPHY 2023 katika viwanja vya gofu,” amesema Brigedia Luwongo

Kwa Upande Meja Japhet Masai, Nahodha wa klabu ya Lugalo, amesema, Shindano hilo kutakuwa na makundi mbalimbali yakiwemo ya wachezaji wa kulipwa, watoto na wanawake.

Naye Girman Kasiga Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa Gofu nchini (TGU), amesema kupitia klabu hiyo, mchezo wa gofu unakuwa kila siku na kwamba wataendele kushirikiana na wadhamini ili kuhakikisha mchezo huo unafika mbali. Wachezaji zaidi ya 100 kutoka klabu mbalimbali nchini wanatarajia kushiriki.

Kwa Upande wake Mkuu wa Idara ya wateja Binafsi wa NMB, Aikansia Muro ambao ni wadhamini wakuu wa mashindano hayo ameishukuru Lugalo Gofu kwa kuwapa nafasi ya kuwa wadhamini wakuu wa Shindano kwa miaka nane mfululizo ikiwa ni miongoni mwa njia za kuwafikia Watanzania.

Habari Zifananazo

7 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button