Mambo yanoga shule Bukoba

Mambo yanoga shule Bukoba

JANUARI 9, 2023 shule zimefunguliwa huku wazazi mitaa mbalimbali  Manispaa ya Bukoba wakionekana kuambatana  na watoto wao wanaoenda kuripoti kwa Mara ya kwanza shuleni.

Licha ya mvua iliyonesha katika mji wa Bukoba leo kuanzia asubuhi,  bado wazazi walionekana kuwa na shauku ya watoto wao kufika shuleni kwa mara ya kwanza, hata muda wa mchana, ili kuhakikisha watoto wao wanapokelewa katika shule walizowaandikisha.

Mwandishi wa HabariLEO ametembelea kata Bakoba na kufika shule ya msingi ya Bunena na shule ya sekondari Bakoba kujionea mwitikio wa wanafunzi wakiambatana na wazazi.

Advertisement

Pia Diwani wa kata Hiyo Shabani Rashidi alikuwa bega kwa bega na uongozi wa shule kwa ajili ya kupokea wanafunzi hao .

“Kuna mvua kubwa lakini niko tayari kuwa na wananchi ambao walinichagua lengo langu ni kuhakikisha watoto wanapokelewa bila kikwazo kwa sababu tayari serikali imejikitika kutuboreshea  miundombinu, tuna madarasa safi na madawati, hivyo hakutakuwa na michango isiyo na tija katika kata hii,”alisema Rashidi.

Taarifa iliyotolewa na  Diwani huyo wa Bakoba, kiasi cha Sh Milioni 220 kimetumika kutekeleza miradi ya elimu katika Kata ya Bakoba, ikiwa utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi chini ya Serikali ya Awamu ya Sita ya  Rais Dk Samia Suluhu Hassan

Alisema ujenzi wa miradi hiyo pamoja kiasi cha Sh milioni  100 zimetumika kukarabati Shule ya Msingi Bunena,  ambapo mpaka sasa ujenzi umefikia asilimia 87, huku ikielezwa kuwa awali shule hiyo ilijengwa kwa tope na kuasisiwa  ujenzi wake  mwaka 1912.

 

Shule ya msingi Bunena baada ya kukarabatiwa.(Picha zote na Diana Deus, Bukoba).

“Ni shule kongwe nchini kwa kipindi cha nyuma shule hii ilikuwa katika hali mbaya hata wazazi waliogopa kuandikisha watoto wao kwa shauku ya majengo kuanguka, lakini uongozi uliopo kwa sasa kuanzia ngazi ya vijiji hadi Taifa.

“Ni uongozi unaoelewa adha ya wananchi wanayopitia sasa Bunena ni shule inayovutia  na Rais Samia ametusikia imeboreshwa majengo, ni ya kisasa wazazi wasibakize mtoto nyumbani,”alisema.

Pia amesema Sh Milioni 120 zimetumika kujenga vyumba sita vya madarasa katika Shule ya Sekondari Bakoba, ujenzi umekamilika na tayari kupokea wanafunzi.

 

Shule ya msingi Bunena kabla ya ukarabati kukamilika.

 

/* */