WAIMBAJI wa nyimbo za Injili Tumaini Akilimali, Joshua Ngoma, Upendo Nkone, Ambwene Mwasongwe, Masi Masilia wanatarajia kupamba Tamasha la Pasaka katika uwanja wa Uhuru Aprili 9 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mwandaaji wa matamasha ya Injili, Alex Msama, mapema leo amesema maandalizi yanaendelea vizuri na kwamba waimbaji kutoka nje na ndani ya Tanzania watashiriki.
“Maandalizi yetu ya tamasha la Pasaka yanaendelea, tamasha hili litakuwa la kihistoria kwa mkoa wa Dar es salaam hii ni baada ya kukaa kwa miaka 7 bila tamasha,” amesema.