MTWARA; MAMALAKA ya Usimamizi Bandari (TPA) mkoani Mtwara imepokea kifaa maalum kwa ajili ya kusaidia meli kuegesha na kuondoka kwenye gati mara baada ya kushusha au kupokea mizigo.
Kifaa hicho maarufu kama Boat Tug chenye thamani ya Sh bilioni 25 kimenunuliwa na TPA kutoka Nchini Vietnam kufuatia agizo la Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha Bandari ya Mtwara, inakuwa na vifaa vyote vya muhimu kwa ajili ya usafirishaji kwenye bandari hiyo.
Akizungumza mara baada ya kupokea boti hiyo, Kaimu Maneja wa Bandari ya Mtwara, Sudi Mwarabu amesema ujio wa boti hiyo kutaongeza na kuleta ufanisi katika utendaji kazi wa bandari hiyo katika kupokea shehana kubwa za mizigo.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala, amesema serikali imewekeza miundombinu ya kisasa katika bandari ya Mtwara ili kuongeza uwezo wa kuhudumia Shehena kubwa.