Mamia wahofiwa kufa maporomoko New Guinea

MVUA kubwa imeipiga milima ya Papua nchini New Guinea, maofisa wa eneo hilo na makundi ya misaada wamesema watu kadhaa wanahofiwa kufa katika maporomoko hayo.

Maafa hayo yaligonga Kijiji cha Kaokalam, Mkoa wa Enga wa Papua New Guinea, karibu kilomita 600 Kaskazini Magharibi mwa mji mkuu wa kisiwa hicho cha Pasifiki Kusini cha Port Moresby, karibu saa 3 asubuhi ya leo Ijumaa.

Kulingana na ripoti kutoka Shirika la Utangazaji la Australia (ABC) na vyombo vya habari vya eneo hilo, watu wapatao 100 wanaaminika kufa, lakini mamlaka hazikuthibitisha takwimu hiyo.

Advertisement

“Mamlaka zinasema kiwango cha maporomoko ya ardhi ni makubwa, lakini bado hawawezi kuthibitisha idadi ya vifo,” alisema Jessica Washington wa Al Jazeera, akitoa ripoti kutoka Jakarta nchini Indonesia.

Ameema janga hilo liligusa jamii ya wakulima walioishi katika eneo la mbali na lenye milima, ambapo maporomoko ya ardhi ni ya kawaida.

Gavana wa Mkoa wa Enga, Peter Ipatas aliiambia Shirika la Habari la AFP kwamba maporomoko makubwa ya ardhi yamesababisha kupoteza maisha ya watu, wanyama na mali katika vijiji sita vilivyoharibiwa na maporomoko hayo.

Waziri Mkuu James Marape amesema ameagiza maofisa kushughulikia uokoaji katika maporomoko hayo.

“Tunatuma maofisa wa dharura, Jeshi la Ulinzi la PNG, na Idara ya Kazi na Barabara kuu kukutana na maofisa wa mkoa na wilaya huko Enga na pia kuanza kazi ya uokoaji, upatikanaji wa miili na ujenzi wa miundombinu, lakini nitatoa taarifa zaidi nitakapojulishwa kikamilifu juu ya kiwango cha uharibifu na hasara ya maisha ya watu,” amesema.

Rais wa Chama cha Maendeleo ya Jamii, Vincent Pyati aliiambia AFP kwamba mvua kubwa ilipiga takribani saa tatu usiku wa jana na inaonekana kama zaidi ya nyumba 100 zilizikwa. Bado haijulikani ni watu wangapi walikuwa katika nyumba hizo.

Elizabeth Laruma, ambaye anaendesha chama cha biashara cha wanawake huko Porgera, mji katika jimbo hilo karibu na mgodi wa dhahabu wa Porgera, aliiambia ABC nyumba katika kijiji cha Kaokalam zilipigwa chini wakati upande wa mlima ulipoanguka.