Mamlaka nchini Tanzania zahaha kuokoa mito inayokauka

PICHA za satelaiti zinaonyesha jinsi ukame mbaya zaidi katika miaka ya hivi karibuni ilivyopunguza kiwango cha maji katika Mto Ruaha Mkuu na vijito vyake ambao umefikia kiwango cha chini zaidi mwezi huu. Wakazi na walioshuhudia wanasema mto huo umekauka kabisa.
Ukataji miti, kilimo na ufugaji vimesababisha vipindi virefu vya ukame katika bonde la Mto Ruaha Mkuu nchini Tanzania ambao hapo awali lilikuwa limejaa maji, yakikitiririka kwa nguvu muda mwingi.
Kihistoria, kwa mara ya mwisho mto huo haukuwa na mtiririko kwa muda mrefu zaidi mwaka 2013 ambapo maeneo kama vile Ibuguziwa yalikauka kabisa.
Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi na Ofisa Mnadhimu katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Godwell Ole Meing’ataki aliliambia gazeti la HabariLEO Jumatatu kwamba “tunachukua hatua.”
Hatua hizo, kwa mujibu wa kamishna huyo, ni pamoja na kuzuia shughuli zaidi za kibinadamu kando ya Mto huo zinazojumuisha malisho ya mifugo na kilimo.
“Tunatengeneza miongozo na taratibu mpya kwa wafugaji,” amesema na kuongeza “Tunataka kuondoa mifugo yote.” Kipindi kirefu cha kiangazi kimeonekana katika bonde hilo huku baadhi ya jamii za Dar es Salaam na ukanda wa Pwani zikihangaika kupata usahihi wa maji.
Meing’ataki amesema kikosi kazi kimeundwa ili kuondoa njia zinazotengenezwa na wakulima kama sehemu ya skimu yao ya umwagiliaji yenye gharama nafuu. Njia hizi za kuchepusha maji zinatoka Mbarali, kupitia Kimani na hadi mto Chimala.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dk.Selemani Jafo amesitisha shughuli zote za kibinadamu katika mto huo mkubwa wiki iliyopita. Alitaka hatua za haraka kutoka kwa mamlaka za mikoa ikiwa ni pamoja na kupanda miti ili kurejesha vyanzo vya maji.
Makamu wa Rais Dk Philip Mpango pia ameagiza watu waliojenga majengo ya makazi karibu na mto huo kubomoa majengo yao na kuondoka eneo hilo. HabariLEO haikuweza kuthibitisha ni watu wangapi wataathirika.
Kiwango cha uharibifu kwenye Mto Ruaha kinakaribia kufanana na mito mingine mikubwa, Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema katika mahojiano.
Waziri Aweso anasema, tathmini ya kitaalamu ya mto huo na ile iliyofanyika katika Mto Ruvu imegundua shughuli kadhaa za uchepushaji na uchimbaji madini ambazo kwa ujumla zilisababisha upungufu wa maji.
“Maji ya Ruaha Mkuu yamekauka, vilevile kwa Mto Ruvu. Hatua madhubuti zisipochukuliwa, nchi itakuwa inakabiliwa na janga hilo hilo kila Novemba. Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani umekumbwa na athari za mabadiliko ya tabianchi. Mikoa hiyo miwili inategemea kwa kiasi kikubwa maji ya Mto Ruvu,” amesema.
Kukauka kwa mto Mto Ruaha kulianza mwaka 1994, kulingana na rekodi rasmi. Tangu wakati huo, Mto umekuwa ukikabiliwa na changamoto hiyo mwaka hadi mwaka. Mto huo ni muhimu kwa uendelevu wa Mradi wa Umeme wa Maji wa Bwawa la Mwalimu Nyerere- mradi unaolenga kuzalisha megawati 2115 za umeme