Man City yahamia kwa Alphonso Davies

MANCHESTER City ipo tayari kutoa pauni milioni 80 kuinasa saini ya beki Alfonso Davies kutoka Bayern Munchen ambaye pia Real Madrid inamtaka, mtandao wa Fichajes wa Hispania unaripoti.

Mkataba wa Davies na Bayern utamalizika msimu wa 2025, kama Bayern itashindwa kumpa mkataba mpya huenda akashawishiwa kwenda City ambao wako tayari kutoa pesa ndefu kwa ajili ya usajili huo.

Real Madrid ina mpango wa kuimarisha upande wao wa kushoto hivyo huenda Davies akawa suluhisho la tatizo la upande huo.

Mpaka sasa Guardiola ameshatumia wacheza kadhaa katika upande huo, ameshamtumia Benjamin Mendy, Oleksandr Zinchenko, Manuel Akanji, Nathan Ake, na Josko Gvardiol lakini hakuna yoyote ambaye amewahi kudumu nafasi hiyo kwa muda mrefu.

Habari Zifananazo

Back to top button