Man City yaingia kwenye rada za Arsenal

KLABU ya Manchester City imewasilisha ofa yake ya kumtaka kiungo wa West Ham United Declain Rice.

Mancity wameripotiwa kuwasilisha dau la Pauni milion 80 pamoja na ongezeko la pauni milioni 10 dili hilo litakapokamilika kitita ambacho kinaweza kuwakosha West Ham United na wakakubali kumpiga bei kiungo huyo wa kimataifa wa England.

Washika mitutu wa London Arsenal walikuwa katika hatua nzuri za kuinasa Saini ya Rice ambapo waliwasilisha ofa ya pauni milioni 75 iliyokataliwa na West ham na sasa wanasubiriwa kurudi na ofa nyingine nono zaidi.

Advertisement

West Ham United wao waliweka wazi yao ya kumuweka sokoni nyota huyo kwa dau la pauni milioni 100 hivyo kinachosubiriwa ni msimamo wao juu ya ofa iliyotumwa na Manchester City lakini pia ofa nyingine itakayowasilishwa na Arsenal.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *