Man, New Castle United kitawaka Wembley

MANCHESTER na New Castle United watavaana kuwania ubingwa wa kwanza katika mchezo wa fainali ya Kombe la Carabao Cup utakaopigwa Uwanja wa Wembley saa 1:30 usiku leo.

Kikosi cha Erik ten Hag kiliitandika Nottingham Forest mabao 5-0 katika mechi mbili za nusu fainali, huku timu ya Eddie Howe ikifika fainali ya kwanza tangu 1999 kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Southampton.

Mashetani Wekundu, ambao wanapigania mafanikio katika michuano minne ya Ligi Kuu, Kombe la FA na Ligi ya Europa pia, hawajashinda taji tangu 2016-17, walipotwaa Kombe la EFL na Ligi ya Europa chini ya kocha wa zamani Jose Mourinho.

Newcastle, ambao walifungwa na Manchester United katika fainali ya Kombe la FA mwaka 1999, watakuwa wakijaribu kushinda taji lao la kwanza kwa takriban miaka 54.

Habari Zifananazo

Back to top button