Man United yakutana na kipigo cha tano

MANCHESTER United imepoteza mchezo wa tano wa Ligi Kuu England, baada ya leo kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa majirani zao Manchester City.

Katika michezo 10 waliyocheza, United imepoteza mitano na kushinda mitano.

Katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Old Trafford, mabao ya City yalifungwa na Erling Haaland mawili na Phil Foden.

Baada ya kipigo hicho, United inashika nafasi ya 8 ikiwa na pointi 16, City iko nafasi ya 3 ikiwa na pointi 24 katika msimamo wa EPL.

Habari Zifananazo

Back to top button