Mandonga kazini leo

MOROGORO: BONDIA Karimu Mandonga leo Desemba 29, 2023 atapanda ulingoni kuzichapa na, Jiti Mawe katika pambano lilopewa jina la Usiku wa Visasi.

Pambano hilo litapigwa mkoani Morogoro likitanguliwa na mapambano mengine mengi huku lengo la mapambano hayo likiwa ni kuinua vipaji vya ngumi vilivyopo mkoani humo.

Mabondia kutoka Morogoro na maeneo mengine watapanda ulingoni kwa ajili ya kutoa hamasa kwa vijana wenye ndoto ya kuishi katika mchezo wa masumbwi iwe kwa kuucheza au kuufanyia kazi nyingine kama vile uamuzi au ukocha.

Kama ilivyo kawaida yake, Mandonga ameendelea kuonesha sanaa ya kuutumia vyema mdomo akimchimba mkwara mzito mpinzani wake na kutamba kumpoteza mapema kabisa kwenye pambano hilo.

Bondia Jiti Mawe nae hajakubali unyonge ametamba kuwa atamvutia pumzi kidogo Mandonga ndipo aoneshe ubora wake na kumfanya Karimu Mandonga kujutia kuzichapa nae.

Habari Zifananazo

Back to top button