Mandonga kuzichapa tena Kenya

Mabondia Karim Mandonga na George Bonabucha wanatarajia kupanda ulingoni kwenye pambano la “Nairobi Night Rumble” linalotarajiwa kufanyika Machi 25,2023 nchini Kenya.

Akizungumza na waandishi wa habari Mandonga amesema anarejea Kenya na ngumi inayoitwa Mlungambuga kutoka Jangwa la Sahara kwenye upepo mkali.

“Ngumi ya Mlungambuga kutoka Jangwa la Sahara itafanya kazi zaidi ya ngumi ya Sugunyo kwenye pambano langu dhidi ya Kenneth Lukyamuzi kutoka Uganda,”amesema Mandonga.

Advertisement

Kwa upande wake Baraka Shelukindo Mkuu wa Masoko Multchoice Tanzania, amesema hii ni nafasi ya kuukuza na kuutangaza mchezo wa ngumi Tanzania na Afrika kiujumla.

Mratibu Msaidizi Bakari Hatibu kutoka kampuni ya Peaktime Sports Agency, amesema wadau wa masumbwi watarajie mazuri kutoka kwao, kwani wanawapa wananchi kinachostahili kupata burudani ya kipekee kwenye mchezo huo.

Mabondia wengine watakaopanda ulingoni kwenye pambano la “Nairobi Night Rumble” George Bonabucha kutoka Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania-JWTZ akizichapa na Michael Dieries kutoka Afrika Kusini, Hassan Ndonga na Nick Otieno kutoka Kenya, Consolata Musanga wa Kenya na Fatuma Yazidu (Tanzania), Zawadi Kutaka na Placedus Oduori wa Kenya

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *