Trending

Mandonga: Nitaleta furaha kwa Watanzania

Bondia maarufu kwa sasa nchini Karim Mandonga, amesema amekusudia kuwapa watanzania furaha baada ya kushinda pambano  kwenye mzunguko wa kwanza (KO) dhidi ya Bondia Mussa Omary.

Mandonga amesema ana mapambano matano na anategemea ushindi wa kibabe. “Nina mapambano matano, hayo yote natarajia niwaletee watanzania furaha. Hivi ndivyo nimeanza na ni tawaletea furaha kubwa zaidi ya hii,” amesema akirejea ushindi alioupata dhidi ya Mussa Omary.

Hata hivyo, Mandoga ametahadharisha kuwa “kuna watu wananibeza ila ipo siku nitaua mtu ulingoni ndio watanzania wajue Mandonga Mtu Kazi.”

Mchezo  huo  wa Sensabika Boxing Match  umeandaliwa ili kuhamasisha watu kushiriki zoezi la Sensa ambalo linatarajiwa kuanza kesho Agosti 23, 2022.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x