MSHAMBULIAJI Sadio Mane anatarajia kufanyiwa vipimo vya afya leo kabla ya kusaini mkataba wa kuitumikia klabu ya Al-Nassr akitokea Bayern Munchen.
Kwa mujibu wa mtandao wa Sky Sport, Mane atakamilisha uhamisho wake kwa dau la pauni milioni £24m.
Mane ataungana na mshambuliaji Cristiano Ronaldo ambaye pia anaitumikia timu hiyo.