KLABU Al Nasrr ya Saudi Arabia inaelezwa ipo mbioni kukamilisha uhamisho wa mshambuliaji Sadio Mane kutoka Bayern Munich ya Ujerumani
Taarifa zinazoenea katika vyanzo mbalimbali barani Ulaya vinasema kwa sasa yamebaki mazungumzo kati ya Mane na Al Nasrr juu ya maslahi binafsi kwani klabu zimefikia makubaliano juu ya ada ya uhamisho.
Iwapo dili hilo litakamilika, ni wazi Al Nasrr itakuwa kati ya timu tishio katika Ligi ya Saudia kwani ataungana na wababe wengine kama Cristiano Ronaldo aliyejiunga mwaka jana miongoni mwa nyota wengine wanaosakata kabumbu huko saudi Arabia.