Maofisa Kilimo wapeni wakulima Elimu- DC Mbogwe

GEITA: MKUU wa Wilaya ya Mbogwe Sakina Jumanne amewataka maofisa Kilimo ndani ya Wilaya hiyo kuwapa elimu ya kilimo bora wakulima ili walime kilimo chenye tija.

Sakina ameyasema hayo leo Oktoba 25, 2023 katika kikao chake na wadau wa kilimo.

Aidha, amewataka maofisa kilimo kuacha kushinda maofisini na badala yake wawatembelee wakulima na kuwapa ushauri muhimu katika kulima hususani katika kipindi hiki cha msimu wa kilimo.

Advertisement

“Acheni kushinda maofisni, wafuateni wakulima muwape elimu ya kilimo, walime kilimo ambacho kitakidhi mahitaji ya biashara na chakula, wasijilimie tu.”Amesema

Katika utekelezaji wa azma hiyo, Halmashauri ya Mbogwe imekwishafanya upimaji wa udongo kwa vijiji 18 vilivyopo ndani ya wilaya hiyo kati ya vijji 387.

Kufuatia hali hiyo, Sakina amewataka wapimaji kuongeza spidi kwenye upimaji wa ardhi kwa kuwa Wilaya ina vijiji takriban 387.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mbogwe Saada Mwaruka, Afisa Kilimo wa Halmashauri hiyo Lawrance Karugaba
ameahidi kazi hiyo kukamilika kufikia January 2024.

Wakati huo huo, Sakina amewatadharisha waliopewa dhamana ya kusimamia upatikanaji wa mbolea kwamba yeyote atakayekwamisha upatikanaji wa mbolea au kuuza mbolea kwa bei ya tofauti kinyume na bei ya elekezi iliyowekwa na serikali hatobaki salama ndani ya Wilaya ya Mbogwe.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *