WAZIRI wa mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amezindua mafunzo rejea kwa maofisa ugani zaidi ya 1000 nchini ambapo amewaagiza kuweka mikakati ya kudumu ya kukabiliana na migogoro ya ardhi inayosababishwa na wafugaji wakati wa kutafuta malisho.
Maagizo hayo yalitolewa jana na waziri huyo wakati akizindua awamu ya kwanza ya mafunzo hayo yaliojumuisha maafisa ugani 120 kutoka mikoa ya Pwani, Tanga, Morogoro na Dar es salaam yaliofanyikaleo Machi 18,2024 mjini Kibaha mkoani Pwani.
Amesema suala la malisho kwa wafugaji limekuwa ni tatizo ambalo limekuwa likizua migogoro ya mara kwa mara baina ya wafugaji na wakulima jambo ambalo linapaswa kushuhulikiwa na maofisa hao kwa kutoa elimu kwa wafugaji.
“Sekta hii ya mifugo inamatatizo makuu manne ambalo kubwa ni suala la malisho, maafisa ugani ni wakati sasa wa kutafuta ufumbuzi wa suala hili, kawaelimisheni wafugaji juu ya umuhimu wa kuwa na maeneo Yao na kuwaandalia malisho mifugo Yao”alisema
Aidha alisema changamoto nyingine ambazo maafisa hao wanapaswa kujishughulikia ni pamoja na ukosefu wa maji, masuala ya matibabu ya mifugo Kwa maana ya chanjo na dawa, na uoatikanaji wa mbegu nzuri za mifugo yenye tija katika uzalishaji.
“Mkasimamie haya ili tuweze kuwa na tija nzuri katika uzalishaji tuache kujisifu tunamifugo mingi na wakati tija ni ndogo serikali imenaendelea kutekeleza mradi wa BBT (Jenga kesho Iliyopo Bora) lengo kuu ni hilo na jingine ni kuongeza ajira kwa vijana wetu wajiajiri,”alisema.