Maofisa ugani waonywa matumizi ya pikipiki

KATIBU Tawala Mkoa wa Lindi, Ngusa Samike, amewataka maofisa ugani mkoani humu kutumia pikipiki zilizotolewa na serikali kwa shughuli za kijamii tu na si vinginevyo.

Sambamba na hilo amewataka maofisa hao kuzitumia pikipiki hizo kwa umakini na tahadhari, ili kujiepusha na ajali ambazo zinaweza kutokea na kugharimu maisha yao.

Samike ametoa wito huo wakati wa ugawaji wa pikipiki 291 ambazo zimetolewa na serikali kwa maofisa ugani mkoani humu.

Akizungumza kwa niaba ya maofisa ugani, Amina Pemba ameshukuru serikali kwa kuona umuhimu wa kutoa pikipiki hizo ili kutatua changamoto ya maofisa hao katika utoaji wa huduma kwa wakulima nchini.

Amesema kwa kutumia  pikipiki hizo, wakulima watapata huduma kwa wakati kwa kuwa uwezo wa kuwafikia kwa haraka umeimarishwa.

Habari Zifananazo

Back to top button