Mapigano yauwa watu 100 Sudan

SHIRIKA la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) limetoa taarifa kuwa watu zaidi ya 100 wameuawa kwenye mapigano katika jimbo la Darfur Kaskazini, magharibi mwa Taifa la Sudan.

Kamishna Mkuu UNHCR, Filippo Grandi ametoa takwimu hizo Juni 16, 2023 na kuongeza kuwa mapigano katika kambi za wakimbizi wa ndani jimboni humo yamepelekea kuuwa idadi hiyo ya watu.

Kiongozi huyo amesema kuwa endapo mapigano hayo yataisha kuna kila dalili hali ikawa mbaya zaidi huku akieleza kuwa UNHCR imepokea ripoti za unyanyasaji wa kingono dhidi ya wanawake na wasichana ndani na pambizoni mwa kambi za IDPs kwenye jimbo hilo lililoko magharibi mwa Sudan.

Advertisement

Hii ni katika hali ambayo, Jumatano Jeshi la Sudan liliwatuhumu wapiganaji wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) kuwa walimteka nyara na kumuuwa Gavana wa jimbo la Darfur Magharibi, Khamis Abdallah Abakar; na kuyataja mauaji hayo kuwa ni “kitendo cha kinyama.”

Umoja wa Mataifa (UN) umelaani mauaji hayo. Vita hivyo vilivyoanza Aprili 15 baina ya wanajeshi wa serikali chini ya Kamanda wa Jeshi la Sudan, Abdel Fattah al Burhan na hasimu wake Kamanda Mohamed Hamdan Dagalo anayeongeza RSF.

1 comments

Comments are closed.

/* */