Marekani kuendeleza misaada Ukraine

RAIS wa Marekani, Joe Biden amesema taifa hilo litandelea kuunga mkono vita kwa kutuma misaada nchini Ukraine huku akiwataka washirika kuendelea kuunga mkono juhudi za vita dhidi ya Urusi.

“Lakini muda unakwenda” Biden alisema Jumapili katika onyo kwa Congress, ambayo imepiga kura kuepusha kufungwa kwa serikali kwa kupitisha kifurushi cha ufadhili cha muda mfupi ambacho kiliondoa msaada kwa Ukraine katika vita dhidi ya Urusi.

“Hatuwezi kwa hali yoyote kuruhusu msaada wa Marekani kwa Ukraine kuingiliwa,” Biden alisema.

“Tuna wakati, sio muda mwingi na kuna hisia kubwa ya uharaka,” alisema, akibainisha kuwa muswada wa ufadhili unadumu hadi katikati ya Novemba.

Biden alihimiza Congress kujadili kifurushi cha msaada haraka iwezekanavyo.

“Wengi wa pande zote mbili – Democrats na Republican, Seneti na House – wanaunga mkono kuisaidia Ukraine na uchokozi wa kikatili ambao unafanywa na Urusi,” alisema katika hotuba kutoka Ikulu ya White House.

Habari Zifananazo

Back to top button