Marekani kuiwezesha NIT umaahili wa barabara

Mkuu wa Chuo cha NIT, Profesa Zacharia Mganilwa Marekani

CHUO cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kipo katika mazungumzo na Mamlaka ya Barabara (FHWA) ya serikali ya Marekani ili kukiwezesha kituo cha Kikanda cha Umaahili katika Usalama Barabarani (RCoE) kufanya tafiti za kina kwa lengo la kupunguza ajali za barabarani.

Akizungumza na waandishi wa habari Jumatatu jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Zacharia Mganilwa Marekani kuiwezesha NIT umaahili wa barabara kuwa maongezi yanaendelea vyema na wanategemea kuingia makubaliano hayo katika wiki chache zijazo.

“Ushirikiano wetu na Mamlaka ya Barabara (FHWA) ya serikali ya Marekani, utasaidia kwa kiasi kikubwa Kituo chetu cha Kikanda cha Umaahili katika Usalama Barabarani kuongeza ubora hasa kwenye eneo la utafiti na mafunzo,” alisema

Advertisement

Mkuu huyo wa Chuo aliendelea kusema kuwa wataalamu kutoka nchini Marekani watakuja kuwafundisha wahadhiri chuoni hapo ambao vilevile wataweza kutoa mafunzo hayo kwa wakufunzi mbalimbali katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Prof Mganilwa alisisitiza: “Lengo kuu la Kituo chetu cha Umaahili wa Usalama Barabarani ni kutoa mafunzo, utafiti na huduma za ushauri zinazohusu usalama barabarani.”

“Mara nyingi kwenye ajali nyingi tumekuwa tukikusanya takwimu za watu walioumia, walio kufa, madereva, madhara yaliyotokea lakini tumekuwa tukisahau kufanya utafiti ili kubaini vyanzo vya ajali. Ni utafiti peke yake ndio utaweza kuwa suluhisho la ajali za barabarani nchini na kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki,” alisema.

Alisema kuwa ufanyaji wa tafiti za ajali mbalimbali utatoa majibu kama kutakuwa na uhitaji wa kufanya mabadiliko ya sheria na kanuni za barabarani.

Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) ni taasisi ya elimu ya juu ya umma iliyoanzishwa mnamo 1975 ili kuweza kutoa mafunzo kwenye eneo la usafiri na usafirishaji.

 

 

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *