MAREKANI imepanga kujenga vituo vitano vya kijeshi katika mradi unaotaka kuimarisha uwezo wa jeshi la taifa la Somalia huku kukiwa na vitisho vinavyoendelea kutoka kwa kundi lenye itikadi kali.
Waziri wa Ulinzi wa Somalia, Abdulkadir Mohamed Nur na balozi wa Marekani, Shane Dixon walitia saini mkataba wa maelewano mjini Mogadishu jana katika kutekeleza mpango huo.
Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayehusika na masuala ya Afrika Molly Phee na Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud pia walihudhuria hafla hiyo.
Makubaliano hayo yanakuja wakati ambapo tume ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika nchini Somalia, inayojulikana kama ATMIS, ilikupunguza uwezekano wa uwepo wake nchini Somalia.