Marekani yagoma kutuma ndege za kivita Ukraine

Rais wa Marekani, Joe Biden amekataa kutuma ndege za kivita za F-16 nchini Ukraine, licha ya wito mpya kutoka kwa maafisa wa Ukraine wa kuomba msaada wa haraka wa vifaa vya anga.

Alipoulizwa na mwandishi wa habari katika mkutano wake jana iwapo Marekani itatoa ndege hizo, Biden alijibu “hapana”.

Kauli yake inakuja siku moja baada ya kiongozi wa Ujerumani pia kukataa kutuma ndege.

Kwa muda mrefu Ukraine imekuwa ikishinikiza washirika wake kutuma ndege za kusaidia Kyiv kuchukua udhibiti wa anga yake katika vita vinavyoendelea dhidi ya Urusi.

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky na maafisa wakuu wa kijeshi wa nchi hiyo wanasema kusiwe na miiko juu ya usaidizi huo wa kijeshi, imeelezwa kuwa Marekani na washirika wake wanahofia suala hilo litasababisha matatizo zaidi kwa kuzingatia Urusi ina silaha za nyuklia.

Falcons F-16 zinazotengenezwa Marekani zinachukuliwa kuwa mojawapo ya ndege za kivita zinazotegemewa zaidi duniani na hutumiwa na nchi nyingine, kama vile Ubelgiji na Pakistan.

Itakuwa uboreshaji mkubwa kwenye ndege za mapigano za enzi ya Usovieti – nyingi zikiwa ni MiGs – Ukraine inatumia hivi sasa, ambazo zilifanywa kabla ya nchi hiyo kutangaza uhuru kutoka kwa USSR mnamo 1991.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x