MARIOO amshukuru Barnaba

MSANII wa Bongofleva, Omar Mwanga ‘Marioo’ amesema, hakuna kitu kigumu kama kushirikiana na wasanii wakubwa kwani mara nyingi wanajiona wako sahihi na hawataki uchangie wazo kwenye kazi yao.

Marioo alisema hayo baada ya msanii Elias Barnaba ‘Barnaba Classic’ kukubali ushauri wake wakati wa kurekodi wimbo wa ‘Marry Me’ ambao ni miongoni mwa nyimbo zilizopata umaarufu mkubwa kwenye albamu ya ‘Love Sounds Different’ na hii imetokana na kusikiliza mawazo ya wengine.

Marioo aliliambia gazete hili jana kuwa anamshukuru Barnaba kwa kumpa nafasi ya kushiriki kwenye albamu yake, lakini pia kukubali ushauri wake wakati wa kuandaa wimbo ‘Marry Me’ kwani kufanya hivyo kunaongeza hamasa na kuifanya kazi iwe bora kuliko ilivyokuwa awali.

“Lakini pia asante kwa kusikiliza wazo langu kwenye hii project maana kuna baadhi ya kaka zetu wengine wakikutumia wimbo wanataka ufanye huo huo hata kama hujapenda baadhi ya vitu.”

Habari Zifananazo

Back to top button