MSANII wa muziki wa bongofleva Omary Mwanga, ‘Marioo’ amesema kuwa msingi wa mafanikio yake ni kujituma na kuwa na muendelezo na kufuata ushauri wa timu yake ambayo imekuwa ikimpa sapoti kwenye kila shughuli yake.
Marioo ambaye anatarajiwa kufanya uzinduzi wa video ya wimbo wa Dear X Kidimbwi Jumapili hii aliyasema hayo Dar es Salaam Alhamis.
Alisema kuwa kutokana na jinsi muziki wa Tanzania unavyozidi kukua na kuzalisha wasanii wengi chipukizi mambo yake yakikaa sawa ana mpango wa kuanzisha lebo yake ambayo itaenda kuwashika mikono wasanii chipukizi kutoka mtaani ambao wamekosa nafasi ya kuonekana licha ya kuwa na vipaji.
“Unajua sisi tunatokea mtaani tunajua machungu wanayokutana nayo watu huko tunakotoka ndio maana tunapenda kuwashika mikono wengine ili kuwafikisha mahala tulipo sisi,” Alisema Marioo.