Marioo, Sho Madjozi Jukwaa moja Dar

DAR ES SALAAM: WADAU wa muziki zaidi ya 2000 wanatarajia kushiriki Kongamano la Pili la Kimataifa la Muziki la ACCES lililopangwa kuanza Novemba 9 hadi 11 jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo Novemba 7, 2023 Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Dk Kedmon Mapana amesema Kongamano hilo litachangamsha uchumi wa nchi kutokana na idadi kubwa ya washiriki kutoka nje.

Amesema tayari serikali imetoa ukumbi wa Mlimani City na kuidhinisha vibali kwa wadau wote wa muziki ambao wameshaanza kuwasili nchini.

Advertisement

“Serikali tunafarijika Kongamano hili litatupatia fedha nyingi za kigeni, watakaa mahotelini, watatengeneza ‘network’, Basata tunalipa baraka kongamano hili kwa mikono miwili.” Amesema Mapana

Amesema, lengo la serikali kuingiza mkono katika tamasha hilo ni kwamba awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hasan imeweka mazingira mazuri na kufungua milango katika tasnia ya sanaa na burudani ambayo inakuwa kwa kasi katika suala zima la kuchangia uchumi.

“Ni sekta iliyoajiri vijana wengi kwa mnyororo wake, msanii kama msanii hawezi kufanya kazi peke yake nyuma yake kuna mnyororo wa watu hivyo inatoa ajira kwa wingi,”mesema Mapana.

Aidha, amesema serikali imetoa ukumbi Mlimani City, Basata imechangia wasanii wote wa nje wanaingia vizuri kwa kuwa tayari wameshaongea na Uhamiaji na kudhamini vibali vyao.

“Tamasha hili linaleta watu wengi kutoka duniani, mambo mengi ya uchumi yatafunguka ndio maana serikali imeweka mkono.

Tunahitaji nchi yetu ya Tanzania iendelee,”amesema.

Aidha, kwa upande wa Mkurugenzi wa Taasisi ya Music in Africa Eddie Hatitye amesema mbali na wanamuziki kutoka mataifa mbalimbali kutumbuiza pia kutakuwa na watoa mada zaidi ya 40 kutoka Afrika na duniani kote, ambao wataangazia mambo muhimu kwenye tasnia ya muziki kitaifa na kimataifa, na namna ya kuukuza, kukuza ujuzi na fursa kwa wadau katika tasnia ya muziki Afrika.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Music in Africa Eddie Hatitye amesema watoa mada zaidi ya 40 kutoka Afrika na duniani kote watashiriki na wataangazia mambo muhimu kwenye tasnia ya muziki kitaifa na kimataifa, na namna ya kukuza ujuzi, kuuza na fursa kwa wadau katika tasnia ya muziki Afrika.

Miongoni mwa watu mashuhuri wataoshiirki kwenye kongamano hilo ni mwanamuziki na mjasiriamali wa Afrika Kusini Sho Madjozi atakayefanya mahojiano na Heather Maxwell wa Sauti ya Amerika, wakati msanii na mtayarishaji wa muziki wa bongo flava kutoka Tanzania Marioo atatoa mada kwenye mkutano huo.

4 comments

Comments are closed.