Marufuku kufunga biashara- Mwigulu

Agizo hilo ni kuanzia Julai Mosi

SERIKALI imepiga marufuku utaratibu  unaochipukia kwa kasi wa taasisi mbalimbali za Serikali na Halmashauri kufunga biashara, ofisi na maeneo mengine ya uzalishaji.

Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba ameyasema hayo leo Juni 15, 2023 Bungeni mjini Dodoma akiwasilisha bajeti ya serikali yam waka 2023/2024

Amesema kumekuwa na tabia baada ya kufanya kaguzi na kuthibitisha ukiukwaji wa sheria mbalimbali zinazosimamia biashara ukimbilia kuzifunga.

“Ufungaji wa biashara, kwa sababu zozote zile, una athari kubwa kwa ustawi wa uchumi wetu kwa kuathiri ajira za wananchi, ustawi wa biashara, mapato ya kampuni na mapato ya Serikali.

”Amesema

Aidha, amesema utaratibu huo unakwenda kinyume na juhudi kubwa za Rais  Samia Suluhu Hassan katika kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini.

Amesema ili kuondokana na athari hizo, anapendekeza kuanzia Julai Mosi, mwaka huu iwe ni marufuku kwa taasisi yoyote ya Serikali kufunga biashara, ofisi ama maeneo yoyote ya uzalishaji kwa kigezo cha kukiuka taratibu mbalimbali.

Aidha, anapendekeza sheria, kanuni na taratibu mbalimbali zirekebishwe ili kumchukulia hatua mwenye biashara kwa makosa ya biashara na siyo kuifunga biashara yenyewe.

“Hatua hii inalenga kulinda ajira za watanzania, mapato ya biashara, kukuza uchumi na kuongeza mapato ya Serikali.

”Amesema

Habari Zifananazo

Back to top button