Marufuku kuondoa wodini wagonjwa wa NHIF

DAR ES SALAAM; Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amepiga marufuku vituo binafsi kuwaondoa wodini wagonjwa ambao ni wanachama wa NHIF, mara baada ya saa 48 kupita tangu kutolewa kwa taarifa ya APHFTA.

Amesema kufanya hivyo ni kuvunja sheria ya madaktari, madaktari wa meno na wataalam wa afya shirikishi Sura ya 152, inayowataka madaktari kutositisha huduma kwa wagonjwa ambao tayari wanawahudumia na wale wagonjwa wa dharura.

“Ninavielekeza vituo/hospitali zote binafsi na za umma nchini kuendelea kuwapokea wagonjwa wa dharura pindi wanapofika katika vituo vyao kwa kuwa hili ni takwa la sheria namba 151 ya usajili wa vituo binafsi vya kutolea huduma na kanuni yake namba 32. Kutowapokea wagonjwa hao ni kuvunja sheria husika,” amesema Waziri Ummy.

Habari Zifananazo

Back to top button