‘Marufuku kutoa fedha upate dhamana polisi’

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo amepiga marufuku utaratibu wa watuhumiwa kutozwa pesa pindi wanapohitaji dhamana, kwani hiyo ni haki yao kisheria.

Kamanda Jongo alitoa marufuku hiyo Machi 19, 2023 wakati akizungumuza na wakazi wa vijiji vya Nzera na Bugando vilivyopo Halmashauri ya Wilaya ya Geita (Geita Vijijini) kwenye mkutano wa hadhara.

Amesema upo utamaduni na imezoeleka kwamba kuingia kituo cha polisi ni bure ila kutoka ni hela, lakini wananchi wanapaswa kutambua huo si utaratibu wa kisheria na hawatakiwi kutoa fedha.

Ameahidi kuwashughulikia maofisa wote wa polisi wanaoendekeza utaratibu huo, huku akiwaelekeza wananchi kumpatia taarifa kwa njia ya simu pindi watakapokutana na vikwazo kupata dhamana.

“Maelekezo yangu mimi Safia Jongo, hakikisha unachotakiwa kufanya ni kupata barua ya mtendaji (mtaa/kijiji) upewe dhamana, akikunyima dhamana nenda hewani kwenye namba yangu ya simu,” amesema.

Habari Zifananazo

Back to top button