JESHI la Polisi Kikosi cha Usalama Barabani limepiga marufuku magari na pikipiki yoyote inayotumika kwa matumizi ya kawaida kufunga ving’ora, vimulimuli, namba bandia na taa za kuongeza mwanga.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Ramadhan Ng’azi amesema kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na wapo baadhi ya wananchi wamegeuza ving’ora kama fasheni katika magari au pikipiki zao.
Kamanda Ng’azi amesema kwa magari au pikipiki kufunga ving’ora, vimulimuli, namba bandia na taa za kuongeza mwanga kwenye magari na pikipiki.
Gari na pikipiki zinazotumika katika misafara ya viongozi, pikipiki za polisi, zimamoto, hospitali na pikipiki za jeshi tena kwa kuzingatia maelekezo ya waziri mwenye dhamana ya usalama barabarani.
“Sheria ya usalama barabarani sura ya 168 kama ilivyopitiwa mwaka 2002 kifungu cha 54 (2) (5), king’ora kutafungwa kwenye gari au pikipiki za dharula tu.” amesema Kamanda Nga’zi.
Jeshi hilo pia limepiga marufuku watu binafsi, makampuni na taasisi kufanya kosa hilo na atakayekiuka agizo hilo anastahili adhabu ikiwemo kulipa faini ya tozo za makosa ya usalama barabarani au kuwekwa mahabusu na kuandaliwa mashtaka kwa ajili ya kufikishwa mahakamani au vyote kwa pampoja.
Kamanda Ng’azi amesema jeshi hilo limeanza operationi nchi nzima ya kukamata magari na pikipiki yaliyofungwa vingora, vimulimuli, taa za kuongeza mwanga (Spot light na Led bar).
Wengine watakaokamatwa katika operationi jiyo ni magari na pikipiki zilizofungwa namba bandia zisizo na usajilie.
Kamanda Ng’azi amefafanua kwamba magari yaliyowekwa taa za kuonheza mwaka kutoka kiwandani yameruhusiwa kwa ajili ya kufanyakazi migodini na uwindaji na si vinginevyo.
“Hizi taa zinapoongezwa mwanga zinasababisha uoni hafifu kwa watumiaji wengine wa barabara pia zinawwza kusababisha ajali hivyo wanaotumia taa hizi kwa kufuata sheria wawe makini na wafuate taratibu na sheria ili waepuke ajali za barabarani.