‘Marufuku wanunuzi pamba kuanzisha vituo binafsi’

BARIADI, Simiyu: Mkuu wa Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu Simion Simalenga amesema katika msimu wa ununuzi wa zao la pamba mwaka huu katika wilaya hiyo, wanunuzi binafsi wa zao hilo hawataruhusiwa kuanzisha vituo vyao binafsi vya kununulia pamba.

Amesema kuwa pamba yote itanunuliwa kutoka kwenye vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS), na wakulima watatakiwa kupeleka pamba yao kwenye vyama hivyo vya msingi ambavyo vipo kwenye maeneo yao.

Simalenga amesema hayo wakati akizungumza na wenyeviti na makatibu wa vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) kutoka wilayani humo wakati wa kikao cha kuweka mikakati ya ununuzi wa zao hilo.

Mkuu huyo wa wilaya amesema wamefikia uhamuzi huo kutokana na msimu wa mwaka jana baada ya makampuni binafsi kuruhusiwa kuanzisha vituo vyao vya kununua pamba lakini wakashindwa kutoa takwimu sahihi za pamba waliyonunua.

“Haya yote yanatokana na kile ambacho tumekutana nacho msimu uliopita mwaka jana, tuliwapa vibali wanunuzi binafsi wakaanzisha vituo vyao, changamoto ikaja kwenye kutoa takwimu sahihi za pamba waliyonunua,” amesema Simalenga…

“ Tumesema safari hii hakuna mnunuzi yeyote ambaye ataruhusiwa au kupewa kibali cha kununua pamba na kuanzisha kituo chake binafsi, pamba yote itanunuliwa kwenye AMCOS,” Simalenga.

 

Habari Zifananazo

Back to top button