Massabo hatanii uwenyekiti ngome ya vijana ACT

NAIBU Waziri Kivuli wa Viwanda na Biashara kutoka ACT Wazalendo, Julius Massabo amechukua rasmi fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya chama hicho katika uchaguzi utakaofanyika Februari 29, 2024.

Katika taarifa yake kwenda kwa waandishi wa habari, Massabo ameeleza misingi muhimu ambayo atafanya mara baada ya kupata nafasi hiyo ikiwa ni kusimamia ngome katika kukamilisha muundo wake (kitaasisi) kwa majibu wa muongozo wa Ngome.

Massabo amesema kuwa atatafuta na kuandaa fursa mbalimbali za mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa ngome ngazi zote nchi nzima.

“Kuimarisha mtandao wa chama vyuo vikuu ili kuwezesha ngome kuwa chemichemi na Tanuri ‘Think tank’ la kupika viongozi na mawazo kwa chama.  Kuhamasiha vijana kugombea kwenye chaguzi za kiserikali ubunge na udiwani ili kuongeza ushiriki wa vijana kwenye ngazi za maamuzi”. Amesema Massabo.

Habari Zifananazo

Back to top button